F Vasco Mgimba aibuka mshindi kwenye kura za maoni Ludende | Muungwana BLOG

Vasco Mgimba aibuka mshindi kwenye kura za maoni Ludende

 



Aliyekuwa Diwani wa kata ya Ludende wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Ndugu Vasco Weston Mgimba ameibuka mshindi wa kura za maoni za wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata hiyo kwa ajiri ya kupata ridhaa ya kuwa diwani.

Mgimba aliyekuwa akitetea nafasi hiyo ameibuka kidedea kwa kupata kura 382 akimshinda mpinzani wake Stephano Weston Luoga aliyepata kura 11 za wajumbe ikiwa katika kata hiyo ni wajumbe wawili pekee waliokuwa wakishindania nafasi hiyo.

Post a Comment

0 Comments