F Talaka chanzo ongezeko la vitendo vya ukatili na unyanyasaji Tanga | Muungwana BLOG

Talaka chanzo ongezeko la vitendo vya ukatili na unyanyasaji Tanga


Miongoni mwa changamoto kubwa inayosabaisha kuwepo kwa unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ni Talaka nyingi ya wazazi kuachana  na watoto kukosa malezi ya pande mbili  jambo ambalo inawakosesha haki ya msingi  watoto wengi.

Hayo aliyasema  sirjent Ruthi Maduhi wakati akizunzungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwenge  jijini Tanga hivi karibuni.

Alisema katika jiji la Tanga utafiti  umeonenyesha watoto wengi wanakumbana na changamoto ya ukatili baada ya wazazi wao kutengena  hivyokusababisawale watoto kulelewa na bibi  au shangazi  ambao wenyewe wako bize hawe kuangalia usalama  wa watoto .

 Kwa upande wake mgeni rasmi Leel Chambo ambaye alimwawakilisha mkurugenzi wa jiji la Tanga Juma Hamsin aliwataka wazazi kuchukua jukumu la kuangalia usalama wa watoto kwa jicho la Tatu ili kuwalinda didhi ya vitendo vya ukatili.

 Alisema katika mkoa wa Tanga vitendo vya ukatili vimekithiri sana lakini  tatizo limeanza kwa familia  wenyewe kuweza kumalizana wenyewe hivyo  ni vyema kuona umuhimu wa kumlinda mtoto ili aweze kufikia ndoto zake.

Awali mwenyekiti wa UHTC, Dkt.Samwel Mturu alisisutiza umuhimu wa kuingilia kati mapema kwa wazazi kutoa kipaumbele ya huduma za afya ,lishe na malezi kwa watoto wenye umri kati ya miaka 0 hadi 8.

"Utoto wa awali ni kipindi nyeti. Ukuaji kamili wa mtoto lazima uanze nyumbani kupitia malezi bora, afya na ulinzi,” alisemaAfisa Mpango wa TAYOTA, Halima Sudi, aliwaonya watoto kutochukua zawadi kutoka kwa watu wasiowajua, akisema hiyo ni mbinu inayotumiwa mara kwa mara na wanyanyasaji.TAYOTA hivi karibuni ilizindua kampeni inayoitwa “Pamoja Tuwalinde”, inayolenga kuimarisha mifumo ya ulinzi na kukomesha utamaduni wa ukimya.

“Changamoto yetu kubwa ni kwamba kesi nyingi haziripotiwi au huachwa njiani kwa sababu ya ukosefu wa mashahidi au maamuzi yasiyo rasmi,” alisema Mkurugenzi wa TAYOTA, George Bwire, katika mahojiano tofauti. “Hili lazima libadilike. Kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali na ushirikishwaji wa jamii kwa nguvu, tunaamini Tanga si tu itaweza kubadili hali ilivyo sasa bali pia kuwa kiongozi kitaifa katika ulinzi wa watoto.”


 

Post a Comment

0 Comments