F Wananchi Lupembe wadai kuwa na matumaini na mgombea wao wamkabidhi tena zigo la barabara | Muungwana BLOG

Wananchi Lupembe wadai kuwa na matumaini na mgombea wao wamkabidhi tena zigo la barabara

 







Wakazi wa Jimbo la Lupembe mkoani Njombe wamemtaka mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Edwin Swalle kwenda kuendelea kupambania changamoto ya barabara ya Kibena - Lupembe - Madeke kwa kiwango cha lami pindi atakaposhinda Ubunge.

Kauli hiyo wameitoa wakati mgombea huyo akichukua fomu ya kugombea Ubunge katika ofisi za Tume huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) huko Kidegembye yaliko makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Njombe huku wakidai kwamba barabara ndio kikwazo kikubwa kwao.

Janan Kinyamagoha,Nickson Kuchungula na Eva Nyato ni wananchi wa Lupembe ambao wanamtaka Swale akishinda tena ubunge katika Jimbo Hilo kuipa kipaumbele barabara hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya Jimbo na uchumi wa wananchi. 

"Kilio chetu cha muda mrefu Lupembe ni barabara na sisi mgombea wetu tunaimani naye,tunatamani iwe kwa kiwango cha lami kwa hiyo tunaamini atamalizia alipoishia"amesema Kinyamagoha

Baada ya kuchukua fomu hiyo mgombea Ubunge Edwin Enosy Swalle anayetetea nafasi hiyo kwa awamu ya pili anasema ataanzia alipoishia katika kushughulikia changamoto za wanalupembe.

"Kwanza ninashukuru CCM kuniamini mimi kwa mara nyingine,nataka niwaahidi nitafanya kazi kwa uamimifu mkubwa sana na nitaendelea kuwa mbunge wa wote kwa sababu ninafahamu kero za jimbo langu na tutaanza tulipoishia"amesema Swalle

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya Wanawake UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela ametumia Fursa hiyo kuwaomba wanawake wote kuungana kukitafutia kura Chama Cha mapinduzi kuanzia Rais,Wabunge na madiwani wote.

Hata hivyo kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi serikali ya awamu ya imekwishatangaza tenda ya ujenzi wa barabara ya Lupembe KM 42 kwa kiwango cha lami ambapo kwasasa anasubiriwa kupitakana mkandarasi ili kuanza ujenzi wa barabara hiyo.

Post a Comment

0 Comments