Na John Walter-Mbulu
Katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jana kwa ajili ya kumpata mgombea wa ubunge wa Jimbo la Mbulu Mjini kwa uchaguzi mkuu wa 2025, aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo, Zachari Paulo Issay, ameibuka na ushindi wa kishindo baada ya kujizolea kura 3,516 kutoka kwa wajumbe wa chama.
Matokeo kamili ya kura hizo za maoni ni kama ifuatavyo:
Zachari Paulo Issay – 3,516 kura
Peter Martin Sulle – 1,435 kura
Baltazari Safari Awe – 987 kura
Andrea Axwesso Tsere – 446 kura
Emanuel Margwe Amma – 34 kura
Kwa matokeo hayo, Issay ameweka rekodi ya kupata kura zaidi ya mara mbili ya aliyemfuatia kwa karibu, akionyesha bado anaungwa mkono kwa nguvu na wanachama wa CCM Mbulu Mjini.
Mchakato huu ni sehemu ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo chama hicho kinapitia hatua za ndani kuhakikisha kinapata wagombea wenye uwezo, uzoefu na kukubalika kwa wananchi.
0 Comments