Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe imewa
onya wagombea watakaoendeleza visasi badala yake imewataka wanachama kuwa kitu kimoja kutafuta kura za Chama cha Mapinduzi.
Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Dkt.Scholastika Kevela mara baada kikao cha baraza kuu la Jumuiya hiyo mkoa wa Njombe kilichofanyika kwenye ofisi za Chama hicho kwa lengo la kuvunja makundi ambayo yalitokana na mchakato wa kura za maoni.
"Ukigombea kuna kura kutosha au kuto kutosha kwa kada wa Chama cha Mapinduzi hata kama kura hazikujaa inatakiwa urudi kufanya kazi za Chama"amesema Dkt.Scholastika
Mwenyekiti ameongeza kuwa "Makundi yote yamekiri kuwa kitu kimoja na kushirikiana kwenda kutafuta kura za CCM kwa ajili ya October 29"
Aidha Dkt.Scholastika amesema katika Baraza hilo wameweza kuwakabidhi madiwani pamoja na wote waliokuwa wamegombea Ilani ndogo ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe ila kwenda kusoma na kuielewa kwa lengo kuzungumza wanachokijua kwa wananchi.
Kwa Upande wake Aziza Kiduda ambaye ni katibu wa UWT mkoa wa Njombe amesema lengo kubwa la kikao hicho ilikuwa ni kuvunja makundi na kwenda kutafuta kura.
"Kikubwa tukatafute kura huku tukiwa mioyo yetu imekunjuka na wamoja badala ya kwenda mtaani huku watu wakiwa wananung'unika"amesema Kiduda
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo Neema Mgaya aliyekuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe pamoja na Rebecca Nsemwa ambaye ni Mgombea Mteule wa Ubunge viti maalum mkoa huo,wamesema kwa sasa hakuna timu na badala yake Jumuiya imekuwa na umoja kama ilivyokuwa awali huku wakiahidi kwenda kufanya kazi za Chama na Jumuiya.