F Wana CCM watakiwa kuvunja makundi ili kusaka kura kwa wagombea wake | Muungwana BLOG

Wana CCM watakiwa kuvunja makundi ili kusaka kura kwa wagombea wake


Na Timothy Itembe Tarime.

MWENTEKITI wa Jumuia ya wanawake Taifa Mery Chatanda amewataka wana CCM  kuvunja makundi ili kuungana pamoja na kutafuta kura za wagombea ndani ya Chama kuamzia Rais Dkt Samia Suluhu Hassani na Mgombea mwenza Balozi DKT Emmanuel Nchimchi,wagombea Ubunge na wagombea Udiwani wa Chama Cha mapinduzi.

Chatanda alisema haijawahi Kutokea Tangu Uhuru Chama Cha Mapinduzi kusimamisha Mgombea Urais mwanamke lakini mwaka huu umetokea kwa Dkt. Samia ambaye amesimama kuomba nafasi hiyo hivyo tunaonba kura nyingi Oktoba mwaka huu na tujitokeze Kwa wingi kumpa kura za kutosha kwa kuwa ametuheshimisha.

Naye Mgombea ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama Cha mapinduzi, Esther Matiko alisema amekuwa Mbunge kupitia CHADEMA Katika Jimbo la Tarime mjini lakini Kwa sasa yupo CCM na kufanya hivyo ataenda kuborresha maisha ya Wanatarime mji kupitia fedha  za mama Samia na kukuza uchumi kwa wa taifa.

Matiko alisema Kwa mkoa Mara wanawake wanne walioteuliwa na Chama kugombea Ubunge wakiwemo viti maalumu Chama kimefikia asilimia hamsini Kwa hamisini ambayo ni sera ya kitaifa na CCM imekuwa mfano wa vyama vilivyosajiliwa vya kisiasa tangu Uhuru haijatokea wanawake wanne kupendekezwa kugombea ubunge.

Mgombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Mwikwabe Waitara alipongeza Vikao vya kamati ndani ya CCM kuwateuwa ambapo Waitara aliomba Kila mama Moja Moja MZITO  pindi atakapo jifungua mtoto amwiite(AMBATIZE) jina Mama Samia Kwa sababu jina Hilo ni la baraka.

Naye Mwenyekiti wa UWT mkoa Mara, Nansi Msafiri alimwagia sifa mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassani Kwa ushirikiano wake na Mwenyekiti wa Jumuia ya wanawake Taifa Mery Chatanda kuwapatia wagombea Ubunge wanawake wanne mkoa Mara.

Nansi alisema hayo Katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama hicho chini ya mwenyekiti wa UWT wilaya Tarime, Neema Newlanda kilichofanyika ukumbi wa CGM Hotel kilichohudhuriwa na makada mbalimbali wa CCM ambapo alisema Kwa kuwateuwa wanawake wanne kugombea ubunge ndani ya mkoa Mara haijawahi Kutokea Tangu uhuru.

Moja ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo, Mery Peter Zakaria aliwaomba wagombea watakapo shinda Vijana wapatowe Ajira Kwa sababu wanahangaika USIKU nachana mitaani wakitafuta kazi.

Mery alisema Vijana wengi wamesoma na wanavyeti wametunza makabatini na masandukuni huku vikiwa vimelala lakini hakuna Ajira"Tunaonba tunaowatuma kwenda Bungeni muwatafutie Vijana Ajira hapo mtakuwa mmewaponya wanawake na Wazazi Kwa ujumla na kazi mtakuwa mmemaliza"alisena Mery.




Post a Comment

0 Comments