Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Mkoa wa Tanga Ustad.Rajab Abdlrahman amewataka wanachama na wagombea waliopita kwenye kura za Maoni kuacha makundi baada ya mchakato kupita kwani umoja ndio utakaoweza kuwapatia ushindi wa kishindo .
Hayo aliyasema wakati wa mkutano mkuu maalumu wa kutafuta kura za wagombea udiwani ,Wabunge na Rais Samia kuputia Chama cha mapinduzi hivyo hukuna sababu ya kujenga tofauti badala yake kuacha makundi kuendelea kutafua kura ili kupata ushindi wa kishindo.
Aidha aliongeza kusema kuwa waliokisaliti Chama wanapaswa kujua Chama Chama cha mapinduzi kinamsimamo hivyo ni kimeamua kushirikiana pamoja lengo kuu ikiwa kuongeza kwa idadi ya kura ndani ya mkoa wa Tanga.
Sambamba na hayo alito wito kwa wale wlioteuliwa kwenye nafasi ya kugombea ubunge au udiwani waache mara moja tambia ya kujitamba mbele ya wale wasioteuliwa ili kuacha kutengeneza makundi vivyohivyo na wale wasioteuliwa wanapaswa kuwa wavumilivu lakini pia kufucha hisia zao ili Chama kisigawanyike.
Kwa upande wake mzee Musa Shekimweri ambaye alikuwa mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa aliwataka wajumbe kuweza kutambua kuwa nafasi ya uchaguzi ni moja tu mtu anapoachwa kwenye kura au kutokueuliwa ni kwaida wala sio jambo la kutengenza chuki na kipindi cha kura za maoni makundi pia kawaida ila baada ya hapo wanapaswa kukaa pamoja na kujenga nyumba moja.
Alisema cha kufahamu ni kwamba wagombea wanaweza kujitokeza wengi kwenye kiti Kimoja lakini baada ya hapo atakayekaa kwenye kiti ni mtu mmoja ambaye ndio atakayebahatika tu hivyo hakuna haja ya kugawanyika ndani ya Chama Cha mapinduzi.
Hata hivyo alitoa ombi kwa viongozi wa CCM kuwa wakati wa Uchaguzi tarehe 29 mwezi October wale wazee wote ambao hawezi kutembea na ni wapiga kura wafuatwe majumbani ila wafike kwenye vituo vya wapiga kura wapige kura zao kuwachagua viongozi wao.
0 Comments