NA REBECCA DUWE TANGA
MWENGE wa Uhuru 2026 umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa upanuzi wa mradi wa Maji na ukarabati wa miundombinu ya maji katika vijiji vya mpapayu,kwakibuyu,kwedunda,magoda ,kicheba na Paramba
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa tenki la Maji lenye ujazo wa Lita 150,000 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026,Wazo Mwang’onda alisema tenki hilo likamilike na wananchi wa kata ya Mpapayu na Magoda waweze kupata maji safi na salama katika maeneo yao ya karibu.
Mradi huo wa ujenzi wa tenki la Upanuzi wa Maji Kata ya unathamani ya Milioni 353,222,150 ambapo utakapokamilika utawahudumiwa watu wapatao 856 na umefikia asilimia 62 ya utekelezaji wake.
Alisema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu alipoingia madarakani aliweka nadhiri ya kwamba wananchi hasa wakina mama anakwenda kuwatua ndoo kichwani wasienda mbali kwenda kuchota maji wayapate katika maeneo yao ya karibu ,
“Katika hili Rais ametimiza jambo hilo na kla mahali wanapokwenda maji yapo vijijini mbali sana maji yapo na leo hapa kata ya Mpapayu na Magoda wamekuja kuweka jiwe la msingi tenki la maji lita 150,000 maji hayo yatatoka kwenye bomba kubwa na kuyaleta maeneo hayai wananchi waweze kupata maji katika maeneo yenu ya karibu”Alisema
Alisema hilo ndio lengo la Rais Dkt Samia Suluhu kumtua mama ndoo kichwani na sasa Magoda na Mpapayu wanakwenda kumtua mama ndoo kichwani muda sio mrefu tenki linakamilika wananchi wanakwenda kupata maji safi katika maeneo yenu ya karibu.
Kiongozi huyo aliwaomba wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu ili nchi ibaki kuwa tulivu ili rais aweze kuwaletea maendeleo makubwa zaidi ya haya wanayaoyaona.
“Ndugu zangu tuendelee kumuomba Rais Dkt Samia Suluhu awe na Afya njema aweza kutuletea maendeleo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona”Alisema
Awali akizungumza Diwani Kata ya Mpapayu alimshukuru kiongozi huyo wa Mwenge 2026 Wazo Mwang’onda kuweka Jiwe la Msingi la Tenki la Maji lenye ujazo wa lita 150,000 kwamba liendee kuendelezwa katika suala la ujenzi.
“ Lakini nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa juhudi kubwa anazozifanya kwa nchi hii hata sisi tuliopo pembezoni mwa mkoa wa Tanga tunaonekana kama sisi hatutambuliwi lakini mama Samia anajicho kali nasi tunatambuliwa na kuona kuna watu wa kata ya Mpapayu ina vijiji vinne na kata jirani yeye vijiji sita Lusanga nao wana umuhimu wa kupata maji safi na salama “Alisema

