Aweka Rekodi ya Kipekee kwa Kuinua Mkono kwa Miaka 53

Kutana na Amar Bharati.


Mtawa huyo wa dhehebu la Sadhu la nchini India, ameinua mkono wake wa kulia, bila kuushusha chini kwa miaka 53 sasa.

Inaaminika kuwa, Bharati alianza kuonesha ishara hiyo toka mwaka 1973, kama ibada kwa mungu wa kihindu, aitwaye Shiva.
Bharati, mwenye umri wa miaka 76, huinua mkono wake wa kulia juu kama ishara ya sala, ya kuombea amani duniani.

Hali kadhalika, Bharati, mwenye umri wa miaka 76, huinua mkono wake wa kulia juu kama ishara ya sala, ya kuombea amani duniani.

Kabla ya mwaka 1973, Bharati alikuwa akiishi jijini New Delhi, na aliajiriwa kama karani wa benki moja huko India.

Bharati, ambaye ana mke na watoto watatu, aliamua kuacha maisha ya kidunia, akiachana na familia yake, na kuamua kumtumikia ‘mungu’ Shiva.

Inadaiwa kuwa, haikua rahisi kwa Bharati kuanza zoezi hilo la kuishi akiwa ameinua mkono wake mmoja juu, kwani alikumbana na maumivu makali katika miaka ya mwanzoni ya kuonesha imani yake.
Inadaiwa kuwa, haikua rahisi kwa Bharati kuanza zoezi hilo la kuishi akiwa ameinua mkono wake mmoja juu, kwani alikumbana na maumivu makali katika mia

Hata hivyo, baada ya miaka miwili, mtawa huyo alianza kuzoea hali hiyo, licha ya mkono wake kufa ganzi na kukakamaa baada ya kukosa mzunguko wa damu kwenye baadhi ya mishipa yake.

Miaka kadhaa baadae, mkono wa kulia wa Bharati ukashindwa kufanya kazi ipasavyo, huku vinganja vyake vikiwa vimekunjana.

Popote aendapo, mkono wa Bharati umeendelea kuwa juu, ishara ambayo ameendelea kuionesha hata akiwa amelala au kufanya jambo lolote lile.

Kwa sasa, mkono wa Bharati unaendelea kuwa juu, na amekuwa kivutio kwenye hija mbalimbali za Wahindu, ambako waumini humshangaa kwa uchaji wake, kwa mungu Shiva.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi