"Hatutaruhusu kufunguliwa kwa njia ya pili kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz" - Iran


Mohsen Rezaei, mshauri wa kijeshi wa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu amesema: "Hatutaruhusu kufunguliwa kwa njia ya pili kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz."

Aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X: "Ikiwa kizuizi kitaendelea, meli na vikosi vya Marekani vitakabiliwa na hatari kubwa na majeruhi."

Kauli za Mohsen Rezaei zinakuja wakati ambapo usafiri wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz bado ni mdogo sana.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema jana (Alhamisi) kwamba anadhani Mlango-Bahari wa Hormuz "upo wazi kwa kiasi fulani" lakini kwamba Iran daima inaweza "kufanya mashambulizi au kutega bomu majini."

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi