Thomas Partey amejiunga na timu ya Ligi Kuu ya Saudi Pro League, Al Shabab, klabu hiyo ilitangaza siku ya Ijumaa.
Kiungo huyo wa Ghana alikuwa hana timu baada ya kumaliza mwaka mmoja akiwa na timu ya Hispania,Villarreal.
Alikuwepo Hispania akitokea Arsenal, ambapo alicheza misimu mitano na kufunga magoli tisa.
Partey alikuwa sehemu ya timu ya Atletico Madrid iliyoshinda taji la Ligi ya Europa 2018. See less
