Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa alibadilisha ndege kwa siri alipokuwa akiondoka kwenye mkutano wa NATO nchini Uturuki mwezi uliopita, kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa tishio la kiusalama.
“Nafuata maelekezo ya Usalama wa Taifa na jeshi. Walitaka nipande ndege nyingine, kwa hiyo nalazimika kufanya wanachoniambia,” Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumanne.
Taarifa hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa Trump alipanda ndege ya Air Force One tarehe 8 Julai mbele ya kamera za televisheni, kabla ya kuhamishiwa kwenye ndege ya kijeshi kwa msaada wa gari la kubeba chakula.
Mabadiliko hayo ya ghafla yameibua maswali kuhusu iwapo watu waliokuwa kwenye ndege iliyotumika kama chambo waliwekwa katika hatari. Hata hivyo, Trump amesema Jumanne kuwa ndege ya kijeshi aliyopanda ilikuwa katika “hatari kubwa zaidi”.Maafisa wameiambia CBS News, mshirika wa BBC nchini Marekani, kuwa Marekani ilikuwa imegundua tishio la kuaminika kutoka Iran la kurusha kombora kuelekea ndege hiyo.
Waandishi wa habari na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani waliokuwa ndani ya ndege hiyo hawakujua kuwa Trump alikuwa ameondolewa kwa siri kupitia mpango maalumu wa kupotosha, kutokana na tishio linalodaiwa kutoka Iran See less
