Maafisa 8 waliokuwa wakihudumu katika meli ya kivita USS Abraham Lincoln wajaribu kujiua


Maafisa wanane waliokuwa wakihudumu katika meli ya kivita ya USS Abraham Lincoln walijaribu kujitoa uhai wakati wa operesheni ya muda mrefu ya kijeshi ya Marekani Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa kaimu Waziri wa Jeshi la Wanamaji la Marekani.

Taarifa hiyo ilitolewa kupitia barua kwa Seneta wa New York, Kirsten Gillibrand, kujibu maswali kuhusu afya na ustawi wa wanamaji waliokuwa sehemu ya msafara huo.

Familia za baadhi ya maafisa hao zimekuwa zikieleza wasiwasi kuhusu kuzorota kwa afya ya akili na mazingira magumu ya kazi wakati wa operesheni hiyo, ambayo ni sehemu ya shughuli za kijeshi za Marekani dhidi ya Iran.

USS Abraham Lincoln imekuwa ikifanya operesheni katika eneo hilo tangu Novemba mwaka jana na kwa sasa iko njiani kurejea Marekani.

Katika barua hiyo, kaimu Waziri wa Jeshi la Wanamaji, Hong Kao, alisema makasisi watano wa kijeshi pamoja na wataalamu kadhaa wa afya ya akili walikuwa wametumwa ndani ya meli hiyo kusaidia mahitaji ya kiroho na kisaikolojia ya wanajeshi.

BBC imewasiliana na Jeshi la Wanamaji la Marekani kwa maoni zaidi kuhusu suala hilo.

Alisema matukio hayo yalihusisha wafanyakazi wa USS Abraham Lincoln pamoja na wanamaji wa kikosi cha anga cha meli hiyo, wanajeshi wa kikosi kazi cha manowari za kivita pamoja na vikosi vyote vya anga vilivyokuwa vimepangiwa kuhudumu ndani ya meli.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi