Marubani wachomana visu ndani ya ndege iliyokuwa ikielekea Israel


Marubani wawili wamepelekwa hospitalini baada ya kuripotiwa kuchomana kwa kisu ndani ya chumba cha marubani wa ndege ya Flydubai iliyokuwa ikielekea Tel Aviv kutoka Dubai.

Ndege hiyo ililazimika kubadili mwelekeo na kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Tabuk, Saudi Arabia, baada ya kutoa ishara ya dharura na tahadhari ya utekaji nyara.

Flydubai imesema abiria wote wako salama

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi