Jumla ya watahiniwa 1,168,649 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kuanzia Septemba 9 na 10, 2026.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohammed amesema kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 531,467, sawa na asilimia 45, huku wasichana wakiwa 637,182, sawa na asilimia 55.
