India ndio “mama wa demokrasia”

 


Katika kongamano la Uchumi lililoandaliwa na Bloomberg mjini New Delhi, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema kuwa India ndio “mama wa demokrasia” wakati ambapo serikali yake inakabiliwa na tuhuma za kuwakamata maelfu ya waliokuwa wakiandamana kwa njia ya amani na kuzuia uhuru wao wa kujieleza.

Takriban wafanyakazi 35 wa vyombo vya habari waliokuwa wakiripoti kuhusu maandamano dhidi ya serikali walikamatwa ndani ya saa 48 mwishoni mwa juma, kulingana na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) yenye makao yake nchini Marekani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi