Rais wa Nigeria aenda Makka kuiombea nchi yake


Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, amesafiri kwenda mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia, kutekeleza ibada ya Umra, ambapo anatarajiwa kuiombea Nigeria, kulingana na taarifa iliyotolewa na ikulu ya taifa hilo.

Msemaji wa Rais huyo , Bayo Onanuga, amesema ziara hiyo itampa rais huyo mwenye umri wa miaka 74 fursa ya kutafakari kiroho, kujitolea katika ibada na kuiombea Nigeria kuwa na amani, umoja, utulivu na maendeleo endelevu.

Tinubu, ambaye ni Muislamu kutoka kusini mwa Nigeria, alisafiri mara ya mwisho kwenda Saudi Arabia kutekeleza ibada ya Umra mwaka 2022, alipokuwa akiwania urais wa nchi hiyo.

Safari ya Tinubu inakuja wakati Nigeria inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwezi Januari, mwaka ujao, huku Nigeria ikiwa inakabiliwa na ukosefu wa usalama hasa kaskazini mwa taifa hilo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi