F KAZI YA INI MWILINI | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

KAZI YA INI MWILINI

INI: Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ni kiungo ambacho kinahitaji kulindwa na kukingwa pamoja na kusafishwa mara kwa mara.

KAZI YA INI MWILINI
1. Ini lina kazi ya uchujaji wa sumu, inachuja sumu kwenye damu ambayo huingia kwa njia ya vyakula, vinywaji (bila kusahau vinywaji vikali), hewa tunayovuta, sigara, pamoja na dawa tunazotumia.

2. Vile vile, hutoa nyongo ambayo kazi yake kubwa ni kusaga mafuta na protini kutoka kwenye chakula tulacho.

3. Pia, ini hukibadilisha chakula na kufanya tupate nguvu mwilini.
Hivyo basi, tunahitaji kulilinda ini ili liweze kufanya kazi yake ya uondaji wa sumu na kusaga mafuta na protini kama ilivyokusudiwa.

Mara nyingi imeonekana kwa mtu mwenye shida ya ini kuwa akijisikia uchovu mara kwa mara hata kama hajafanya kazi za kuchosha.

Hii tutokea kwa kuwa ini limezidiwa na haliwezi kufanya kazi yake ya kuhakikisha mwili unapata nguvu.

VYAKULA VINAVYOLINDA NA KUSAFISHA INI
1. Kitunguu saumu: Inasaidia ini kutoa viashiria ambavyo husaidia kuondoa sumu kwenye mwili, pia husaidia kulilinda ini lisiharibiwe na sumu.

2. Green tea: Inaondoa mafuta kwenye ini na kulifanya ini kufanya kazi inavyotakiwa, vilevile husaidia kuondoa sumu kwenye ini.

3. Mboza za majani: hasa spinachi, husaidia kuondoa sumu hasa zile zitokanazo na mionzi, au matumizi ya vitu vya electronic kama vile simu nk.

4. Parachichi husaidia kulilinda ini lisiharibiwe na sumu

5. Dalansi (lipo kama chungwa, ni kubwa kwa umbo, lina rangi kama pink au nyekundu kwa ndani)

6. Limao: kwa mtu ambaye hana tatizo la vidonda vya tumbo anaweza tumia limao.