FAIDA 10 YA JUISI YA UKWAJU

Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU. 

  • Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets
  • Andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu   baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni  uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu 
  • Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe  andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe 
  • Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.


FAIDA YA JUISI YA UKWAJU. 

  • Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  • Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  • Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  • Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  • Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  • Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  • Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  • Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  • Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  • Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla

Watu waishio bara la Asia, Carribian na America ya kusini,wanajua kuwa kula ukwaju maana yake ni Afya Njema.

Ukwaju unaoliwaa katika maeneo haya maeneo hayo una faida nyingi kwa watu wanaoula.
Kwa hiyo siku nyingine unapoenda kufanya manunuzi ya vyakula hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi. Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na faida za kiafya za ukwaju. 

Ukwaju una ladha faluni ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.

Katika nchi kama Jamaica, Mexico, Aruba na India, ukwaju unachanganjwa na sukari na kuuzwa kama pipi katika mitaa na madukani. Kula ukwajua au bidhaa zitokanazo na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema.

Lakini kati ya faida zingine nyingi za virutubisho na kiafya za ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni za muhimu zaidi, na ni kama zifuatazo:

  1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. Ukwaju una carotenes, Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.
  2. Ukwaju unakuepeusha na ukosefu wa Vitamini C.
  3. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua.
  4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni.
  5. Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.
  6. Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.
  7. Ukwaju unapunguza cholesterol mwilini.
  8. Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema.
  9. Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.
  10. Ukwaju ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe Kwa Tanzania ukwaju unapatikana kwenye masoko karibu yote. 
    Ninakushauri kutengeneza juisi ya ukwaju nyumbani kwako na weka sukari kidogo na juisi hiyo iwe sehemu ya chakula chako. Kama wewe unapenda kula hotelini au kwenye vioski basi agizo juisi ya ukwaju ikusaidi kushushia chakula.