F Makumbusho na nyumba ya Utamaduni Yaandaa onyesho la Uhuru wa Tanzania | Muungwana BLOG

Makumbusho na nyumba ya Utamaduni Yaandaa onyesho la Uhuru wa Tanzania

Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam imeandaa onyesho maalumu linaloelezea mtiririko mzima wa namna uhuru ulivyopatikana, ili kutoa nafasi kwa Watanzania na watu mbalimbali waweze kujikumbusha na kujifunza mambo mbalimbali yanayahusu uhuru wa Tanzania.

Mkuu wa Idara ya Programu katika makumbusho hiyo Chance Ezekiel amesema imekuwa ni utaratibu wa kila mwaka kwa makumbusho ya Nyumba ya Utamaduni kuwa na programu zinazoendana na matukio ya kitaifa ambapo mwaka huu wameona waweke onyesho la uhuru ili kuwarithisha wanafunzi misingi muhimu iliyowekwa na waasisi wa taifa hili.

Wanafunzi kutoka shule mbali mbali wamepata nafasi ya kuona onyesho hilo na wao kufanya sanaa mbalimbali zinazoelezea misingi ya uhuru wa Tanzania ambapo wazazi nao walipata nafasi ya kulizungumzia onyesho hilo.

Kwa mujibu wa Chance Ezekiel onyesho hilo litadumu kwa muda wa mwezi mmoja hivyo watu mbali mbali wanakaribishwa kwenda Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam mkabala na chuo cha IFM kujionea na kujifunza mengi juu ya Uhuru wa Tanzania.