F Pongezi za AY na Babu Tale kwa Mwana FA | Muungwana BLOG

Pongezi za AY na Babu Tale kwa Mwana FA

Hapo jana msanii wa Bongo Fleva, Mwana FA aliteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).

Watu mbalimbnali kutoka kwenye kiwanda cha muziki Bongo wamempongeza Mwana FA, miongoni mwao ni AY na Babu Tale ambao wametumia kurasa zao za Instagram kufanya hivyo.

"Msomi toka Tanga tunakutegemea uko ulipo ila uwe unawaleta mabinti kucheza home utakuja uza mabarafu uzeeni we haya.," ameeleza Babu Tale.

Kwa upande wake AY ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi zaidi na Mwana FA amemshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Mwakyembe kwa uteuzi huo.

"Ahsante Mheshimiwa Harrison Mwakyembe kwa kuona Mwana FA anafaa kuwa Mjumbe mmoja wapo wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa. Naamini Mabadiliko CHANYA mengi tutayaona All the Best Champ," amesema Mwana FA.

Mwana FA ameteuliwa pamoja na msanii wa filamu Single Mtambalike maarufu kama Rich, pia na wajumbe wengine watatu.