F Zitto Kabwe aitwa na TAKUKURU | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zitto Kabwe aitwa na TAKUKURU

 Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU Bregadia Jenerali, John Mbungo amemtaka Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe, kufika ofisini kwake kwa mahojiano zaidi kuhusiana na taarifa aliyoitoa katika mitandao ya kijamii kuwa makampuni matatu ya Chuma ya China yamewahonga baadhi ya watendaji wa serikali.

Taarifa hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari kwenye barua iliyoandikwa na Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU Bregadia Jenerali John Mbungo, ambayo imeweka wazi juu ya kupata kwa taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe juu ya uwepo wa rushwa kwenye makampuni ya chuma.

Baada ya barua hiyo kumfikia mwenyewe Zitto Kabwe, ametumia ukurasa wake wa twitter kuijibu na kusema ataitikia wito huo, huku akiwataka TAKUKURU kuweka wazi taarifa zote atakazowapa na kuzifanyia uchunguzi.