https://monetag.com/?ref_id=TTIb Hivi Pesa ni nini? | Muungwana BLOG

Hivi Pesa ni nini?

Habari za muda huu mpenzi msomaji makala haya, bila shaka u mzima na unanendea vyema na majukumu yako ya kila siku. Naomba nikukaribishe jamvini tuweze kujifunza kwa pamoja kuhusu nidhamu pesa.

Hivi Pesa ni nini?
Maana wapo wengine wamekuwa wakiita majina tofauti tofauti, wapo wale wanaosema ya kwamba pesa ni sabuni ya roho, wapo wengine wanaosema pesa ni mvunja sheria, wapo wanaosema ya kwamba pesa ndiyo kila kitu na maneno mengine kama hayo.

Lakini pesa hiyo hiyo imekuwa na majina tofauti tofauti  hii ni kutokana na sehemu tofauti tofauti ambapo pesa hiyo hutumika, ukienda mashuleni  wanasema ni ada, kwenye gari ni nauli, ukienda kwenye majumba ya ibada huita ni sadaka au zaka, kwingineko huita ni miala, wengine pia walikwenda mbali zaidi na kuita ni bili, achilia hao ambao walikwenda mbali zaidi, wapo  wale walikwenda jirani waliita ni mishahara, wapo wengine ambao waliita ni kodi na maneno mengine kama hayo. Kwa kifupi  hayo yote humanisha pesa.

Lakini licha ya kuwa na hizo pesa, wapo wale wenye nazo, hawa kwa jina moja tunawaita matajiri. Lakini wapo wale ambao hawana pesa, hao nao kwa mkunyasiko wao huwa tunawaita  maskini, watu hao nadhani somo hili ndilo ambalo linawahusua zaidi.

Swali hili liwaende hasa hasa wale ambao hawana pesa, na kila mmoja wao ajihoji yeye mwenyewe ni kwa nini mimi sina pesa?

Miongoni mwa kanuni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu ili aweze kuishi maisha yenye mafanikio husasani katika kipengele cha umiliki wa fedha ipo haja na sababu ya muhimu sana ya kuweza kuitambua na kuiheshimu sana fedha.

Nasema hivyo nikiwa na ushahidi ulio waza kabisa ya kwamba si kila mmoja wetu anaifahamu vyema pesa. Hii ni kwa sababu wapo baadhi ya watu wakipa fedha wamekuwa ni watu wa kuponda mali kufa kwaja.

Kwa muktadha huu utaona ni kwa jinsi ipo haja ya kila mtu kuweza kuifahamu pesa kiundani.

Kwanza kabisa yapo mambo matano unayopaswa kuyafahamu kusiana na pesa;

1. Unatakiwa uzielewe vyema pesa.
Pesa ni vitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, hata hivyo kila kitu ili uweze kukitumia vyema ni lazima ukielewe vyema. Huwezi ukasema uanata kuendesha gari wakati hufahamu kitu chochote kusiana na gari, hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe.

Kama ilivyo kwenye gari, harikadharika katika pesa ni vivyo hivyo. Kwanza kuna falsafa mbili ambazo husimama dede katika pesa. Ili pesa iweze kumfikia mtu kuna viingiza pesa na vitoa pesa.

Hivyo ili uweze kuwa na nidhamu ya pesa ni lazima uje ya kwamba viingiza pesa ni lazima view vichache kuliko vitoa pesa. Kanuni hii ndiyo ambayo imekuwa ikiwashinda watu wengi zaidi. Wao  wemekuwa na vitoa pesa vingi kuliko viiingiza pesa.

Kwa maneno mengi tunaweza kusema labda  ya pesa ni mashetani hii ni kwa sababu tumekuwa hatuzifanyi pesa hiyo vitu vya maana na imekuwa ikiisha ghafla bin vuu.

Lakini ukweli ni kwamba pesa si mashetani kama ambavyo wengi vinywa vyao husema bali  sisi wenyewe ni visababishi ya pesa hiyo kuwa hivyo. Maana yangu ni  kila mmoja wetu atafute vyavyo vingi vya kumuingizia pesa kuliko kuwa matumizi mengi. Hata hivyo kila wakati ni lazima ikumbukwe ya kwamba  kama Matumizi yakizidi mapato huo ni umaskini wa standard geuge.

2. Tengeza mazingira ya kujilipa mshahara.
Miongoni mwa kanuni muhimu inatayokusaidia wewe kuweza kuiheshimu pesa ni pamoja na kuwepo kwa mazingira  thabiti ya kujilipa mshahara kwa kila kazi ambayo unaifanya. Kanuni hii inawahusu wale wote ambao wameajiriwa na wale wote waliojiajairi pia.

Kwa mfano kwa yule ambaye ameajiliwa na analipwa mshahara wa shilingi laki moja mara baada ya kuigawa pesa yako katika mafungu matano, basi  unashauriwa kugawa tena fungu la sita ambalo hili litakuhusu  wewe kuweza kujilipa mshahara. Hapa unaweza kukadiria mwenyewe ya kwamba unajilipa kiasi gani.

Harikadharika wewe uliyejiajili vivyo hivyo unatakiwa kujiwekea utaratibu wa kujilipa mshahara. Kitendo hiki utakifanya mara baada ya kujua unaingiiza kiasi gani kwa mwezi na? na unatakiwa kujilipa kiasi gani?.

Pia unashauriwa kiwango hicho cha mshahra ambacho unajilipa ni lazima ukiwe sehemu salama na unaweza kuweka katika fixed account.

Kwa maneno mengine tunaweza tukasema kiwango hiki cha mshahara ambacho unajilipa  tunaweza tunakiita mafao binafsi. Lakini ikimbukwe pia kiwango hicho cha mshahara kisiwe na mahusiano na pesa yako ya akiba kwani hivi ni vitu viwili tofauti.

3. Weka akiba.
Nidhamu ya pesa bila ya kujua somo la kuweka akiba ni sawa na bure. Hivyo ili uweze kuona pesa inakwenda sawa kama vile ambavyo unataka wewe ni muhimu sana kuweza Kujua na kutambua umuhimu wa kuweka akiba.

Somo hili la uwekaji wa akiba huweza kuwafanya matajiri wengi kuendelea kubaki kwenye chati ya mafanikio kila mwaka, hii ni kwa sababu wengi wao wamekuwa wanaiheshimu sana pesa, na si kuiheshimu tu bali mara baada ya kupata pesa huwa wanatenga asilimia kadhaa ambapo huiweka katika fungu la akiba.

Hivyo hata wewe ndugu yangu kwa kiwango chochote kile cha pesa unachokipata unashauriwa kuwezaa kutenga walau 15% kwa ajili ya kuweka akiba. Kuweka akiba ni muhimu  sana kwa sababu humsaidia mtu hasa pale anapokuwa ameishiwa kabisa , au pale ambapo jambo lolote la dharula linapojitokeza mbele yake.

Hivyo kila wakati ni muhimu kuweza kutambua ya kwamba akiba ni muhimu sana katika maendeleo ya maisha yako.

Na. Benosn Chonya