Wachezaji 20 Yanga SC waifuata Namungo FC


Mapema Asubuhi ya leo kikosi cha Yanga SC kimesafiri kuelekea Lindi kwenye mchezo wa kombe la ASFC dhidi ya Namungo FC utakaochezwa siku ya Jumapili.

Msafara umejumuisha wachezaji 20, benchi la ufundi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili na Mashindano, Hussein Nyika.

Safari hiyo ni baada ya kurejea hapo jana Dar es Salaam wakitokea mkoani Mwanza ambapo walicheza mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Mbao FC na kuibuka na ushindi wa goli 2-1.