F Azali Assoumani apata ushindi wa kishindo Comoro | Muungwana BLOG

Azali Assoumani apata ushindi wa kishindo Comoro


Rais wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili.

Matokeo yaliyochapishwa na tume ya uchaguzi jana jioni, yamempa Azali ushindi wa kishindo wa asilimia 66.77 ya kura.

Kwa ushindi huo Azali Assoumani amemwacha mbali mpinzani aliyekuja katika nafasi ya pili, Mahamoudou Ahamada ambaye kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa ameambulia asilimia 14.62 ya kura zilizopigwa, na kwa maana hiyo haitahitajika duru ya pili.

Lakini hata kabla ya matokeo hayo kutangazwa tayari upinzani ulikuwa umekwishayapinga ukidai kuwa upigaji kura uliandamwa na kasoro nyingi ambazo ziliripotiwa na tume ya uchaguzi.

Upinzani huo ulizilinganisha kasoro hizo na mapinduzi dhidi ya serikali, na kutoa wito kwa umma kusimama kidete na kuipinga hali hiyo.Mahamoudou Ahamada alikwenda mbali na kuitaka jumuiya ya kimataifa kutoutambua ushindi wa Azali.