Ticker

6/recent/ticker-posts

 


China yapinga kuingizwa siasa kwenye uendelezaji wa mtandao wa 5G


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Geng Shuang amesema kuingiza siasa kwenye uendelezaji, matumizi na ushirikiano wa mtandao wa 5G na hata kufanya suala husika kuwa la kisiasa na kuchukua hatua za ubaguzi sio tu hakusaidii maendeleo ya 5G, bali pia kunakwenda kinyume na kanuni ya ushindani wenye usawa na kutolingana na maslahi ya pamoja ya jamii ya kimataifa.

Habari zinasema Marekani na Poland jana zilisaini "taarifa ya usalama wa 5G", ikisisitiza kuwa katika mchakato wa ujenzi wa mtandao wa 5G, nchi zote zinatakiwa kuchagua kampuni ambayo inaaminiwa, haimilikiwi na serikali, ina muundo wazi wa umiliki, kufuata maadili na kanuni za biashara na kufanya shughuli za kibiashara chini ya usimamizi wa mfumo wa sheria ulio wazi. Taarifa hiyo haikutaja jina la kampuni yoyote, lakini vyombo vingi vya habari vimesema Marekani imetaka washirika wake ikiwemo Poland isiruhusu Huawei kushiriki kwenye ujenzi wa mtandao wa 5G.

Akizungumzia taarifa hiyo, Bw. Geng amesema China inaitaka Poland ifuate ahadi yake kwamba itaitendea kampuni ya China kwa usawa na haki na haitachukua hatua ya kibaguzi dhidi ya nchi au kampuni fulani, pia kuitaka Marekani irekebishe kosa lake la kutumia vibaya maana ya usalama wa taifa, kuacha kuharibu jina na kutoa shutuma dhidi ya China na kuacha kuikandamizi kampuni ya China bila ya sababu yoyote.

Wakati huohuo, kampuni ya Huawei imetoa taarifa ikisema kwa muda mrefu, serikali ya Marekani sio tu imeshawishi serikali za nchi mbalimbali kupiga marufuku matumizi ya vifaa vya Huawei, bali pia imetumia njia mbalimbali haramu kuathiri shughuli za kawaida za Huawei na washirika wake.