F Mcheza Tenesi Muaustralia Nick Kyrgios afungiwa kwa wiki 16, kisa? | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mcheza Tenesi Muaustralia Nick Kyrgios afungiwa kwa wiki 16, kisa?


Nyota wa Tenisi kutoka Australia Nick Kyrgios jana alipokea adhabu ya kufungiwa kwa wiki 16 na ATP na amewekwa kwenye uangalizi kwa miezi sita baada ya kuonesha tabia chafu na utovu wa nidhamu uwanjani mwaka mmoja uliopita.

Adahabu hiyo imeambatana na masharti yakiwemo kutafuta usaidizi wa mtaalamu anayeshughulikia tabia katika kipindi atakachokuwa akitumikia adhabu yake.

ATP imesema adhabu ya kufungiwa itaondolewa baada ya miezi sita ya uangalizi kumalizika endapo atatimiza masharti aliyopewa.

Mwezi uliopita aliwahi kupigwa faini ya dola za kimarekani 113,000 kwa matumizi mabaya ya mpira, kuondoka uwanjani bila ruhusa, kutumia lugha ya matusi na kuonesha dharau baada ya kushindwa na Mrussia Karen Khachanov katika michuano ya Cincinnati Masters.