F Yanga yadai kupoteza ya Mamilioni fedha, wailima Bodi ya Ligi barua | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Yanga yadai kupoteza ya Mamilioni fedha, wailima Bodi ya Ligi barua


Yanga SC imeeleza masikitiko kufuatia kuhamishwa kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons kutoka Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya hadi Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli akizungumza baada ya kuhamishwa kwa mchezo huo amesema wamewaandikia barua Bodi ya Ligi ili kujua gharama za kuhamisha mchezo zitalipwa na nani.

"Tumefika Iringa saa saba usiku na Tanzania Prisons wamefika saa 3 Usiku na tumetumia gharama kubwa pale zaidi ya milioni 18 ambayo ni milioni 6 ka siku na tumekaa zaidi ya siku tatu", ameongeza Bumbuli

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo katika dimba la Samora mjini Iringa, ukiwa ni mchezo wa pili kwa Yanga katika Nyanda za Juu Kusini baada ya kucheza na Mbeya City na kutoa sare ya bila kufungana.

Ikumbuke kuwa achezo huo ulihamishwa kutokana na kuharibiwa kwa Uwanja wa Sokoine kufuatia tamasha la muziki lililofanyika katika uwanja huo usiku wa Disemba 25 mwaka huu.