Tetesi za soka leo Mei 28


Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, ametoa ombi la kibinafsi kwa klabu ya china ya Shanghai Shenhua, la kutaka kurefusha mkataba wake wa mkopo Manchester United. (Manchester Evening News)

Liverpool wanataka kumsaini winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 24, huku mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp akiripotiwa kuwasiliana na mchezaji huyo moja kwa moja. (TodoFichajes - in Spanish)

Muda wa David Luiz Arsenal unaelekea kukamilika baada ya kubainika mkataba wa kiungo huyo wa Brazil wa miaka 33- unakamilika mwezi ujao. Mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanzinshwa kuhusu mkataba mpya. (Sky Sports)


Liverpool haitalipa ada ya £50m itakayomwezesha mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, kujiunga nao wakikadiria kuwa thamani yake ni £30m katika soko la sasa la uhamisho. (Mirror)

Beki wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, huenda akajiunga na Chelsea kwa ada ya £22.4m. (Telegraph - subscription required)

Tottenham wanapania kuwapiku washindani wao kadhaa wa ligi ya Premia katika usajili wa winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26. (Football Insider)


Beki wa Newcastle Mhispania Javier Manquillo, 26, anataka kujiunga na klabu ya La Liga club nchini kwao mkataba wake utakapo kamilika mwezi ujao. (Newcastle Chronicle)

Manchester United na Real Madrid wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Rennes Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Metro)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho klabu hiyo "haitatumia fedha nyingi" awamu ijayo ya uhamisho wa wachezaji. (Sky Sports)


Arsenal na Tottenham wanang'ang'ania kumsajili kwa mkataba wa bila malipo kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unakamilika msimu huu. (Telegraph)

Newcastle imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, baada ya Bayern Munich kubadili nia ya kumpatia mkataba wa kudumu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mundo Deportivo - in Spanish)


Newcastle wanamlenga kiungo wa kati wa Liverpool Xherdan Shaqiri, 28, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguli tena msimu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswizi amewakilisha klabu hiyo mara 10 tu msimu huu. (Mail)

Manchester City wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaka kinda wa Ajax Sontje Hansen, 18, ambay alishinda tuzo ya Golden Boot katika kipute cha kombe la dunia kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 msimu uliopita. (Goal)