Jun 1, 2020

Baada ya Mwanafunzi kuuawa kanisani Wanigeria wataka haki itendeke

Kuna ghadhabu nchini Nigeria baada ya mauaji ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22, Uwavera Omozuwa aliyeuawa kanisani.

Kampeni ya hashtag #JusticeForUwa au # HakiKwaUwa imeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria, huku familia yake ikiomba msaada wa kumtafuta aliemuua.

Uwavera alikua anajisomea katika kanisa "tulivu" karibu na nyumbani Benin City wakati alipouawa, dada yake, Judith, aliiambia BBC idhaa ya Pidgin.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi alikufa hospitalini siku ya Jumamosi, siku tatu baada kushambuliwa.

Judith Omozuwa alisema kuwa dada yake alibakwa.

Familia yake ilisema kuwa ilipokea simu kutoka kwa mwanamke kutoka kanisa la Redeemed Christian Church of God siku ya Jumatano jioni.

Uwavera alipelekwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata, sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imejaa damu, Judith Omozuwa alisema.

'Kushindwa kukabiliana na unyanyasaji wa jinsia '

Hatahivyo, msemaji wa polisi katika jimbo la southern Edo, ambalo mji mkuu wake ni Benin City, ameiambia BBC Idhaa ya Pidgin kwamba wanashughulikia tukio hilo kama mauaji, si kesi ya ubakaji.

Mwanafunzi huyo aliuawa kufuatia mapigano katika kanisa, msemaji aliongeza, bila kutoa maelezo zaidi.

Uwavera alikua ndio tu amedahiliwa katika Chuo Kikuu cha Benin kusoma microbiolojia.

Mara kwa mara alikwenda kukaa na "kusoma" katika kanisa karibu na nyumbani kwao kwasababu kulikuwa na utulivu, dada yake aliongeza kusema.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa katika vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa kikundi cha wanaume kiliingia kanisani na kumbaka na baadae kumgonga na kifaa cha kuzima moto (fire extinguisher).
KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger