Na Paschal D.Lucas,Mwanza
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Lyoma Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza Ndugu Kasalali E.Mageni (CCM) ameibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa kupata Jumla ya kura 138 akifuatiwa na Ndugu Bujaga Moses Charles aliyekuwa na kura 131 huku namba tatu ikishikiliwa na ndugu BusigaSolwe M.Shinje aliyekuwa na kura 110.
Uchaguzi huo wa kura za maoni ulikuwa na Jumla ya Wagombea 78 na ulifanyika katika ukumbi wa Kanisa katoliki Parokia ya Nyambiti.
Wilaya ya kwimba ambayo ina Majimbo mawili ambayo ni Sumve na Kwimba ambapo katika Jimbo la Kwimba uchaguzi wa kura za maoni unatarajiwa kufanyika leo Julia, 21,2020.
Ikumbukwe Jimbo la Sumve lina miaka 25 tangu lianzishe na limeshikiliwa na Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi chote na Mbunge wake alikuwa Marehemu Richard Mganga Ndassa aliyefariki April 29,2020 Jijini Dodoma.