Jul 3, 2020

Timu ya simba yaanza safari leo kuwafuata Namungo

KLABU ya Simba imeanza safari leo, Julai 3, kuelekea Lindi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa Julai 8.

Baada ya mchezo huo Simba itakabidhiwa kombe baada ya kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2019/20 ambalo litakuwa ni la kwao jumla baada ya kulitwaa mara tatu mfululizo.

Walianza msimu wa 2017/18,2018/19 na msimu huu wa 2019/20 hivyo kwa mujibu wa kanuni watabaki nalo kwenye makabati yao.

Simba itaivaa Namungo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye mchezo wake uliopita walipokutana Uwanja wa Taifa alikubali kufungwa mabao 3-2.

Hivyo utakuwa ni mchezo mgumu kwa kuwa Uwanja wa Majaliwa Namungo wamekuwa bora kwenye mechi zake alizocheza hapo ambapo ni Coastal Union pekee iliambulia ushindi.

Yanga ililazimishwa sare Machi 15 na Azam FC iliacha pointi tatu ilipotua Uwanja wa Majaliwa.
KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger