Iran yamshikilia kiongozi wa upinzani kwa tuhuma ya shambulizi la 2008

Iran imesema jana kuwa kitengo chake cha ujasusi kinamshikilia Jamshid Sharmahd, kiongozi wa kundi ambalo linatuhumiwa kuhusika na shambulizi la bomu la 2008 na pia kushiriki katika majaribio mengine kadhaa, mwenye makazi yake nchini Marekani .

Taarifa ya wizara ya usalama iliyonukuliwa katika televisheni ya umma, haijasema kwa jinsi gani, wapi au lini kuzuiliwa huko kulifanyika.

Taarifa hiyo ilisema Sharmahad alipanga na kuongoza shambulizi la kwenye kituo cha kidini katika mji wa kusini wa Shiraz. Watu14 waliuawa na wengine 215 walijeruhiwa.