Aug 2, 2020

Polisi 18 wamejeruhiwa katika maandamano ya Berlin

  Muungwana Blog 2       Aug 2, 2020
Jumla ya polisi 18 wamejeruhiwa wakati jeshi hilo likilitawanya kundi kubwa la watu waliokuwa wanaandamana kupinga hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona mjini Berlin, Ujerumani.

Kupitia ukurasa wake wa twitter polisi inasema maafisa wake watatu walipaswa kwenda kupatiwa matibabu hosipitali.

Polisi iliusambaratisha mjumuiko huo, ambao ulihudhuriwa na takribani watu 20,000, katika mazingira ambayo waandaaji walishindwa kutoa hakikisho la hatua za usalama.

Idadi kubwa ya waliohudhuria maandamano hayo hawakuvaa barakoa au kuzingatia kanuni ya kujitenga.

Polisi ya mjini Berlin ilisema ilipeleka askari 1,100 katika tukio hilo la jana kufuatilizia hali ya mambo na kuutawanya umma.

logoblog

Thanks for reading Polisi 18 wamejeruhiwa katika maandamano ya Berlin

Previous
« Prev Post