Aug 2, 2020

Waziri Kabudi awataka wakulima nchini kulima miti dawa

  Muungwana Blog 2       Aug 2, 2020


Na Farida Saidy, Morogoro.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Paramagamba Kabudi amewataka Wakulima hapa Nchi kulima Miti na Mimea Dawa itakayosaidia katika kutibu Magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza na yanayoambukiza kama Ugonjwa wa Covid 19 ambao umetokomezwa hapa Nchi kwa kutumia miti dawa hiyo.

Amesema miti dawa kama Mfumbasi na mingine imesaidia katika kupambana na kutokomeza kabisa wa ugonjwa wa covid 19 nchini,hivyo amewataka wakulima na Watanzania kwa ujumla kuwekeza nguvu kubwa  katika kupanda miti hiyo katika maeneo yao.


Waziri Kabudi ameyasema hayo Mkoani Morogoro wakati akifungua maonesho   ya Wakulima nanenane kanda ya mashariki na kueleza  kuwa kanda hiyo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Nchi kwani imejitosheleza katika sekta zote kama usafirishaji,uvuvi,utalii na Kilimo ambapo amesema kwa Mkoa wa Morogoro pekee unauwezo wa kuzarisha mazao ya kila aina.

Aidha amewapongeza wakulima wa Tangawizi na Malimao hapa Nchi kwa kuwa wazalendo katika kipindi cha ambacho Taifa lilikuwa linapamba na Ugonjwa wa Covid 19 kwa utopandisha bei ya mazao hayo ambayo yalikuwa yanawasaidia watanzania katika kujinginga na Ugonjwa huo.

Kwa uapnde wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo amewataka wakulima wa Korosho kanda ya mashariki hususani wa Mkoa wa Pwani kusafisha na kupuliza dawa ambazo zinazopatikana kwa urahisi katika maeneo yao  ili kujikinga  na Magonjwa mbalimbali katika zao hilo na kupata Korosho zenye ubora.

Katika hatua nyingine amewataka wakulima wa Mikoa ya Pwani,Tanga na Morogoro kulima zao la Mkonge ili kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla na kuondokana na dhana ya kuwa zao la Mkonge ni zao ambalo linalimwa na Taasisi na mashirika makubwa hivyo kila Mtanzania anauweza wa kulima na kumiliki shamba la Mkonge hapa Nchini.

Kanda ya mashariki inaundwa na mikoa ya Morogoro,Pwani Dar Es Salaam Na Tanga ambapo kwa mwaka huu zaidi ya washiriki mia tano na ishirini na sita (526)wameshiriki katika maonesho ya wakulima nanenane katika viwanjwa vya Mwalim Julius Nyerere Manispaa ya Morogoro ambapo yanafanyika maonesho hayo kikanda kila Mwaka.

logoblog

Thanks for reading Waziri Kabudi awataka wakulima nchini kulima miti dawa

Previous
« Prev Post