Oct 16, 2020

Lipumba aahidi neema kwa wananchi wa Mbeya

  Muungwana Blog       Oct 16, 2020

 


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha wananchi,(CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa atahakikisha anaongeza upatikanaji wa umeme nchi nzima kwa kufua umeme wa megawatt 100 mpaka 200 kwa kutumia mradi wa makaa ya mawe yanayopatikana Kiwira wilayani Kyela mkoani Mbeya.


Profesa Lipumba, amesema mradi wa kufua umeme kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwira ni mradi ambao hauchukui muda mrefu, hivyo serikali ingeweza kuongeza upatikanaji wa umeme nchi mzima kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwila.


Ameongeza kuwa mradi huo wa umeme ungeweza kusaidia kwa haraka wakati serikali inajipanga kupata fedha za kukamilisha mradi wa Bwawa la Nyerere, kwani mradi huo umeanzishwa kwanza badala ya kutekelezwa kwanza.


''Wakati tunajipanga vizuri kupata fedha za kukamilisha mradi wa stiegler's Gorge, haya ni mapungufu ya serikali ya CCM, hakuna sababu kwanini ule mradi wa kufua umeme wa megawatt 200 mpaka 300 kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwila mpaka hivi sasa bado haujatekelezwa", amesema Profesa Lipumba.

logoblog

Thanks for reading Lipumba aahidi neema kwa wananchi wa Mbeya

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment