Oct 14, 2020

Tetesi za soka kimataifa

  Muungwana Blog 3       Oct 14, 2020


 Barcelona wanaandaa kuwanasa nyota wawili Pogba na kiungo wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 27, anaendelea kuungwa mkono na wenzie ndani ya Manchester United licha ya kueleza shauku yake ya kuichezea klabu ya Real Madrid. (Manchester Evening News)

Leeds United wanamuania kiungo wa Norwich City na timu ya England chini ya miaka 21, Todd Cantwell, 22, pamoja na kiungo wa Derby County na England chini ya miaka 19 Louie Sibley, 19. (Yorkshire Evening Post)

West Ham na Brentford zimekubaliana kuhusu uhamisho wa £30m wa mshambuliaji Said Benrahma, 25, lakini bado kukubaliana maslahi binafsi na mshambuliaji huyo wa Algeria. (Sky Sports)

Klabu ya Championship Middlesbrough imeweka mkakati wa kumnasa mlinzi wa kushoto wa England na Tottenham Danny Rose, 30, mpaka kufikia Ijumaa jioni. (Football Insider)

Mlinda mlango wa Manchester United Muargentina Sergio Romero, 33, anataka kuvunja mkataba mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu, akitaka kuhamia ligi ya Marekani. (Sun)

Crystal Palace wanakaribia kukamilisha uhamisho wa mkataba mfupi wa beki wa kulia Nathaniel Clyne, 29, ambaye ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kuondoka Liverpool kwenye majira ya joto. (The Athletic)

Cardiff na Swansea zinapambana kuwania saini ya kiungo wa Liverpool na Wales Harry Wilson, 23, kwa mkopo wa muda mrefu (Wales Online)

Kiungo wa Manchester United na Hispania Juan Mata, 32, alikataa ofa ya mshahara wa £200,000 kwa wiki kutoka timu ya Saudi Arabia. (Sport)

Mlinzi wa Sevilla na timu ya Ufaransa chini ya miaka 21 Jules Kounde, 21, anawaniwa na Manchester United kuelekea dirisha la usajili la mwezi January. (ESPN)

Mshambuliaji wa zamani wa Italia na timu za Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 30, ambaye yuko huru sasa baada ya kuondoka Brescia, atasainiwa kwenye klabu mpya ndani ya wiki chache zijazo. (Goal)

West Brom wanakaribia kukamilisha usajili wa £14m wa mshambuliaji wa Huddersfield Town muingereza Karlan Grant, 23. (Football Insider)

Winga wa Derby County, muholanzi Florian Jozefzoon, 29, yuko kwenye mazungumzo na Rotherham United. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Switzerland Shani Tarashaj, 25, amerejea Everton baada uhamisho wake wa mkopo kwenye kikosi cha Uholanzi cha FC Emmen kuvunjwa (Liverpool Echo)

logoblog

Thanks for reading Tetesi za soka kimataifa

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment