Oct 16, 2020

Trump na Biden wakabiliana katika mdahalo wakiwa vituo viwili tofauti

  Muungwana Blog       Oct 16, 2020

 


Wagombea wakuu wa urais nchini Marekani, Donald Trump wa Republican na Joe Biden wa Democratic, wamejitokeza katika vituo viwili tofauti vya televisheni. 


Katika mdahalo huo kila mmoja amemtuhumu mwenzake, juu ya namna anavyouchukulia ugonjwa wa COVID-19, sambamba na siasa za ndani na za kimataifa. 


Kwa wengi, mahojiano hayo yamechukuliwa kama duru ya pili ya mdahalo wa uso kwa macho kati ya Trump na Biden, ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika jana, lakini Trump akajitowa baada ya waandaaji kuamuwa ufanyike kupitia mtandao, kufuatia Trump kuuguwa COVID-19 wiki mbili zilizopita.


 Akihojiwa na kituo cha televisheni cha ABC mjini Philadelphia, Biden alisema Trump hajayachukulia kwa umakini zaidi maradhi hayo, ambayo yashawaangamiza Wamarekani zaidi ya laki mbili.

logoblog

Thanks for reading Trump na Biden wakabiliana katika mdahalo wakiwa vituo viwili tofauti

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment