Nov 24, 2020

Vyombo vya habari binafsi vyakataa kurusha hotuba ya Museveni


Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliagiza Vyombo vyote vya Habari kurusha hotuba yake kila Jumapili saa moja hadi saa tatu usiku ila Muungano wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari umekataa.

Muungano huo umekataa agizo hilo wakisema katika msimu wa kampeni hawawezi kutoa fursa kwa mgombea mmoja pekee bila kuzingatia wagombea wengine.

Kulingana na Sheria ya Utangazaji ya Uganda ya mwaka 2013, kila mgombea anastahili kupewa nafasi sawa katika Vipindi na Habari zinazochapishwa au kupeperushwa na Vyombo vyote vya Habari nchini humo.

Msemaji wa Museveni, Don Wanyama, alitangaza kuahirishwa kwa hotuba hiyo baada ya Vyombo vya Habari kukataa kurusha hotuba hiyo.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger