China kuwawekea vikwazo maafisa wa Marekani wanaojihusisha na Taiwan

 


China imesema hii leo kwamba itawawekea vikwazo maafisa wa Marekani waliojihusisha na kile walichokiita tabia mbaya kuelekea Taiwan ambayo China inadai ni eneo lake. 

Matamshi haya yanatolewa baada ya Washington kuondoa vizuizi vya kimahusiano kati ya maafisa wake na wa Taiwan.

Mahusiano baia ya nchi hiyzo yamezidi kuzorota, wakati China ikiwa imelaani hatua hiyo ya Marekani iliyotangazwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo, katika siku za mwishoni za utawala wa rais Donald Trump. 

China imesema suala la Taiwan ni tete kabisa katika uhusiano wake na Marekani, na tayari iliimarisha shughuli zake za kijeshi karibu na kisiwa hicho, ambazo ni pamoja na kurusha ndege za kijeshi karibu na kisiwa hicho, ikiwa ni moja ya hatua zake za kujibu kuongezeka huko kwa mahusiano kati ya Marekani na Taiwan.


Post a Comment

0 Comments