Jan 18, 2021

Fountain Gate Academy wajipanga kufanya mageuzi katika soka la wanawake hapa nchini

 


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Mkurugenzi wa Fountain gate academy ambao pia ni wamiliki wa timu za Fountain gate wanaume inayoshiriki ligi daraja la kwanza na timu ya Tanzanite wanawake  inayoshiriki ligi kuu ya wanawake amesema wamejipanga kuhakikisha wanaisuka timu ya wanawake ili iweze kufanya vizuri katika ligi inayoendelea baada ya kuanza vibaya ligi.

Amesema timu ya wanawake imekuwa haifanyi vizuri katika ligi hivyo kwa sasa wamesajili wachezaji wazuri ili wafanye vizuri na malengo yao ni kushika nafasi tatu za juu katika ligi.

"Wote mnafahamu timu tumeinunua  mda umeisha hatukuweza kufanya lolote ndio maana mwanzo wa ligi timu imefanya vibaya lakini sasa tuko siliazi na mpira tunataka kufanya mageuzi katika soka" amesema Makao.

Amesema katika kuimarisha timu hiyo wamepata wadhamini watano ambao watasaidia katika kuendesha timu hiyo ili kuamusha ali kwa wachezaji wafanye vizuri katika ligi na kutoka katika nafasi mbaya.

Amewataja wadhamini hao kuwa ni Corie super rice ya Morogoro, UBA Banki ambao watajikita kwenye kudhamini mchezaji bora wa mwezi na kununua kila bao linalofungwa kwa shilingi elfu hamsini(50,000), Simba nazi, Jeff Solutions na Fountain gate academy.

Nae afisa habari wa timu ya Fountain gate academy Juma Ayo ametaja wachezaji waliosajiliwa katika kuongeza nguvu ni Aquila Gasper(beki), Stella Wilbart (kiungo), Saada Ramadhan (kiungo) wote kutoka timu ya Simba Queen, Merry Masatu, (beki) Anna Ebron wote kutoka Ruvuma, 

Wengine ni Zuhura Waziri (kipa) na Madeline Augustino (beki) kutoka Ilala ambao hao wamesajiliwa katika kipindi cha dilisha dogo kuongeza nguvu katika timu hiyo.

Ametumia mda huo kuwataka wakazi wa jiji la Dodoma kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika mchezo utakaowakutanisha timu ya Tanzanite( Fountain gate princess) na timu ya Bao bao Queens mchezo wa ligi kuu ya wanawake utakaochezwa katika uwanja wa Fountain gate arena.

Pia timu hiyo leo imetambulisha jezi zao mpya za tatu zitakazotumika katika michezo yao baada ya awali kutambulisha jezi za nyumbani na ugenini tu.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger