JPM asimulia Maalim Seif alivyookoa ndoa Zanzibar

 


Rais wa amhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amempongeza Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kukubali kuwa miongoni mwa viongozi wa serikali inayoongozwa na Dkt Mwinyi na kwamba maamuzi yake yaliokoa ndoa  ya watu.


Kauli hiyo amneitoa hii leo Januari 14, 2020, mkoani Geita, mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo na viongozi hao wawili waliomtembelea nyumbani kwake Chato, na kuongeza kuwa maamuzi ya Maalim Seif yalikuwa ya kishujaa na yenye mwongozo waMungu na kwamaba mwanga wa maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana.


"Zipo ndoa ambazo zilivunjika hasa kule Pemba, labda mwanamke aliipigia kura CCM na mwanaume akapigia ACT, na siku Maalim Seif ameingia kwenye serikali ndoa zile zikaungana, hii maana yake maamuzi yake yameunganisha wana ndoa na yana baraka kwa Mungu", amesema Rais Dkt. Magufuli.


Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa, "Maalim Seif nataka nikuhakikishie uko kwenye serikali ambayo utaitumikia kwa moyo wako mwema na usishangae siku nyingine nikakualika kwenda kufungua mradi wowote na bahati nzuri nimepigiwa kura nyingi tu Zanzibar na mimi napanga ziara ya kwenda Pemba na Unguja kuwashukuru".

Post a Comment

0 Comments