Jan 14, 2021

Kiongozi mwandamizi wa KMC FC afariki dunia

Kiongozi  Mwandamizi wa Timu ya KMC FC ndugu, Raphael Waryana amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi 

Ndugu Waryana atakumbukwa kwa mchango wake  mkubwa ambao alikuwa akiutoa katika Timu ya KMC FC ikiwa  ni pamoja na ushirikiano wake katika kipindi ambacho Timu ilipokuwa ikitimiza majukumu yake.

Aidha uongozi umeshtushwa na taarifa hiyo na kuahidi kuendelea kuuenzi mchango wake mkubwa aliokuwa anautoa kwa Timu wakati wa uhai wake.

Uongozi unatoa pole kwa familia yake, mashabiki wa Timu ya KMC FC na Umma wa wanamichezo na kuwaomba wawe na  uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wetu.

 

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger