RAS Lindi awataka watendaji na maofisa tarafa kuwafutilia wanafunzi wasio jiunga na elimu ya sekondari




Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Katika kuhakikisha watoto waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2021 wanaanza masomo. Katibu tawala wa mkoa(RAS) wa mkoa wa Lindi, Rehema Madenge amewataka watendaji wa vijiji, mitaa, kata na maofisa tarafa wahakikishie wanafunzi hao wanaripoti katika shule za sekondari walizochaguliwa kujiunga. 


Madenge ametoa agizo hilo jana mjini Nachingwea kwenye sherehe za kuwapongeza wadau wa elimu wa wilaya ya Nachingwea kwa kuwezesha wilaya hiyo kuwa na matokeo mazuri ya ufaulu wa mitihani ya shule za msingi na sekondari kwa miaka mitatu mfululizo. 


Madenge ambae alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo zilizoandaliwa na halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, alisema kiwango cha wanafunzi walioripoti na kuanza masomo hakiridhishi. Kwani hadi sasa idadi ya walioripoti ni chini ya asilimia arobaini na tano.

Alisema nijambo lisilokubalika kuona juhudi za serikali zinashindwa kuzaa matunda kutokana na wanafunzi kushindwa kuripoti shuleni. ¥ Katibu tawala huyo wa mkoa wa Lindi alibainisha kwamba serikali inatumia gharama kubwa kuboresha miundombinu. Ikiwamo vyumba vya madarasa. 

Kwahiyo haipo tayari kuona wala kusikia juhudi hizo zinakwamishwa. 

'' Serikali imeingia gharama kubwa kujenga vyumba vya madarasa na mambo mengine katika sekta ya elimu. Sasa kwanini watoto wasisome? Hali hii ikiachwa kunaweza kuwa na madarasa yasiyona wanafunzi,'' alisema Madenge. 


Kwakuzingatia ukweli huo, amewataka watendaji na maofisa hao wawatafute wanafunzi wasio ripoti ili wapelekwe shuleni. 

Mbali na hayo, katibu tawala huyo ametaka miradi ikamilike kwa wakati, viwango na isimamiwe kikamilifu. Huku akiweka wazi kwamba kutokamilisha miradi kwawakati kunatoa tafsiri kwamba hakuna uhitaji

Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ni miongoni mwa halmashauri  kumi nchini zilizoongeza kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka kwa muda wa miaka mitatu mfululizo. Ambapo katika halmashauri hizo kumi, halmashauri hiyo ya Nachingwea ipo nafasi ya nane. 

Post a Comment

0 Comments