Jan 14, 2021

TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa kesho

 


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa itakayonyesha kesho Ijumaa Januari 15, 2021 huku siku zinazofuata zikitarajiwa kuwa shwari hadi Januari 18.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Alhamisi Januari 14, 2021 inaeleza kuwa utabiri huo wa siku tano kuanzia leo unaonyesha mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini.


Tahadhari hiyo ya mvua kubwa imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tabora, Singida, Dodoma, Ruvuma, Mahenge, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe huku uwezekano wa kutokea kwa utabiri huo ukiwa wa wastani.


“Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji,” inaeleza taarifa hiyo ya TMA.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger