Jan 18, 2021

Wanaoshindwa kulea watoto waandaliwa sheria


Na Amiri Kigalila,Njombe

Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe kupitia afisa lishe  imesema inaandaa sheria ndogo ili kukabiliana na wazazi na walezi ambao wanashindwa kuwalea watoto wao ipasavyo na kusababisa tatizo la udumavu.

Afisa lishe Rahel Magafu amesema hayo mara baada ya kutoa elimu ya lishe bora kwa wananchi wa mtaa wa Itebetala uliopo kata ya Mjimwema,ambapo amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni wazazi hususani baadhi ya wanawake kujihusisha na tabia ya unywaji wa pombe hali ambayo inasababisha muda mwingi wawe vilabuni na kushindwa kuwahudumia watoto kwa kuwapa chakula bora.

Aidha amesema kuwa sheria hiyo ndogo ambayo itatungwa itaenda kuwabana na akina baba ambao wanashindwa kushirikiana na wake zao katika malezi ya watoto ikiwemo na tabia ya kushindwa kuhudhuria cliniki ili kuona maendeleo ya mtoto wake.

“Tumetoa malekezo kwenye serikali za mitaa,serikali za kata kuunda sheria ndogo zikazowabana wakina baba waweze kushiriki kikamilifu katika malezi na matunzo ya watoto,changamoto nyingene ni ulevi uliokithiri unakuta mchana saa 8 hata akina mama wapo kwenye vilabu na watoto mgongoni,sheria ndogo tunazitunga ambazo zitawabana hawa walezi”alisema Rahel Magafu

Afisa ustawi jamii katika halmashauri ya mji wa makambako SOPHIA PREMO amesema changamoto ya akina baba kushindwa kushiriki katika malezi na makuzi ya watoto ni kubwa na amewataka watambue kuwa wajibu wa kuwalea watoto ni wajibu wao.

“Wazazi wengi wako bize sana kutafuta pesa hatukatai lakini kikubwa wahakikishe ulinzi na usalama wa motto unakuwepo”aliseama Sophia Premo

Akizungumzia kuhusiana na namna ya kukabiliana na tatizo la udumavu katika mji wa Makambako mhudumu wa afya ngazi ya mtaa wa cheresi CHRISTER MLIGO,amesema kuwa wazazi na walezi wanatakiwa kuzingatia makundi ya vyakula ambayo wanawapa watoto wao na waachane na tabia ya kuchanganya nafaka  za aina moja na kuita ni unga wa lishe.

Hata hivyo baadhi ya wanawake wa mtaa wa Itebetala wamesema kuwa serikali inatakiwa kuendelea kutoa elimu hiyo ya namna ya uundaaji wa chakula bora kwa watoto ili kukabiliana na tatizo la udumavu ambalo lipo katika mkoa wa njombe.

Mkoa wa Njombe unatajwa kuongoza kitaifa kwa kuwa na tatizo la udumavu ambapo watoto wenye udumavu chini ya miaka mitano inatajwa kufikia asilimia 53.6.


 

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger