Feb 23, 2021

Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya viongozi wawili zaidi wa kijeshi Myanmar


Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya viongozi wawili zaidi wa utawala wa kijeshi nchini Myanmar na kuonya kuchukua hatua zaidi wakati mamia kwa maelfu ya watu wakikaidi onyo la mamlaka na kuendelea na maandamano ya kudai kurejeshwa demokrasia ya nchi hiyo. 

Marekani imesema inazuia mali yoyote inayomilikiwa nchini Marekani na kuwazuia kuingia nchini humo maafisa wawili wa Baraza tawala la Taifa -- Jenerali Maung Kyaw, anayesimamia jeshi la angani na Luteni Jenerali Moe Myint Tun. 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Anthony Blinken amesema Marekani ametoa wito kwa jeshi na polisi kusitisha mashambulizi yote dhidi ya waandamanaji, kuwaachia huru mara moja waliokamatwa kinyume cha sheria, kusitisha mashambulizi na vitisho dhidi ya wanahabari na wanaharakati na kurejesha serikali iliyochaguliwa kidemokrasia. 

Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya Umoja wa Ulaya pia kuidhinisha vikwazo dhidi ya jeshi la Myanmar.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger