Feb 23, 2021

Nchi za Magharibi zaendelea kuishinikiza Myanmar

 


Nchi tajiri za kundi la G7 zimelaani vitendo vya kupewa vitisho na kukandamizwa watu wanaopinga mapinduzi yaliyofanywa na jeshi nchini Myanmar. 


Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 wamesema matumizi ya nguvu dhidi ya watu wanaoandamana kupinga mapinduzi ya Myanmar hayakubaliki na wahusika wanapaswa kubebeshwa dhamana. 


Katika taarifa yao ya pamoja mawaziri hao wamelaani vitendo hivyo wakisema wataendelea kuwa na mshikamano katika kulaani mapinduzi ya Myanmar. 


Kadhalika wametowa mwito wa kuachiliwa mara moja bila ya masharti watu wote waliofungwa ikiwemo kiongozi wa serikali iliyochaguliwa na raia Aung San Suu Kyi pamoja na rais Win Myint. 


Aidha Umoja wa Ulaya nao umesema unafikiria kuiwekea vikwazo nchi hiyo wakati Marekani ikiwawekea vikwazo majenerali wawili wengine zaidi kwa kuhusishwa na mapinduzi hayo ya kijeshi.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger