Feb 19, 2021

Rais Magufuli atangaza siku tatu za maombi

 


Rais wa Tanzaniwa John Pombe Magufuli amewataka Watanzania Wakristo na Waislamu kumuomba Mungu ili kuepuka ugonjwa ambao amesema mwaka jana ''Tuliushinda kwa kumtanguliza Mungu''. Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Katibu Mkuu kiongozi John Kijazi.

'' Ulipoingia ugonjwa huu wa kubana mafua mwaka jana tulimtanguliza Mungu pamoja na juhudi zingine mbalimbali, unapoona kitu huwezi kukitatua wewe muombe Mungu'', amesema Magufuli.

Marehemu Kijazi alifariki dunia baada ya kuugua na anatarajiwa kusafirishwa hadi Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi siku ya Jumamosi

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger