Feb 23, 2021

Waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda washutumiwa kuhusika na kifo cha Balozi wa Italia Nchini DRC


Balozi wa Italia Nchini DRC, Luca Attanasio aliuawa katika shambulio Februari 22. Serikali imewashutumu waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda kwa shambulio hilo

Balozi Attanasio alikuwa katika msafara wa Shirika la mpango wa Chakula Duniani (WFP) na walishambuliwa karibu na Mji wa Goma, mashariki mwa Congo

Hata hivyo, kundi la FDLR limekanusha kuhusika na shambulizi hilo kwa kile inachosema vikosi vyake viko mbali na eneo la shambulizi

Maafisa katika Mbuga ya Wanyamapori ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara lililoshindikana, pale walipoingilia kati mara moja


KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger